Msaada Kupata Mtaji Kuanzisha Biashara
Halo jamani, natumai wewe ni mzima wa afya Jina langu ni, Hamis Ally Athumani kutoka Dar es Salaam Tanzania. Nilizaliwa tarehe 01/11/1992 Elimu yangu ni ya Msingi, darasa la saba Niko katika uhusiano wa ndoa, na tumefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume.
Hivi sasa ninafanya kazi kwenye App ya Taxi Online, ambapo hapo awali nilifanya kazi kwa Teknolojia za Moovn Kwanini nimekuja hapa, kwa sababu ya kile nilicho nacho ninaamini kupitia nguvu ya Umma ninaweza kupata msaada kufikia malengo yangu ambayo ninao.
Kama kijana mwenye lengo la kutaka kusonga mbele kibiashara na kuweza kutoa ajira kwa watu wengine kupitia biashara yangu hii naomba msaada wako ili kuniwezesha kupata Mtaji wa kuendeleza biashara yangu hii.
Kama inavyoonekana kutoka kwenye picha, hapo ndipo ninapofanya biashara yangu, nimefanikiwa kulipa ushuru wa pango kwa miezi sita na kumaliza vibali vyote kutoka kwa serikali na sasa nimeanza biashara yangu ya kuuza nafaka, kwa mfano; Mchele, Maharagwe, Unga, kunde, Karanga, n.k.
Lengo langu kuu, biashara hii ya kuuza nafaka ni kufikia hatua ya kuuza kupitia wateja tofauti pamoja na mtandaoni, hapa tayari nimeunda akaunti ya Instagram na Facebook inayojulikana kama @homenafakashop Home Nafaka Shop ina chapa kamili, mifuko na nembo yake ambayo utumia kubeba bidhaa.
Kupitia wateja hawa wa mtandaoni nitakuwa nikitoa huduma ya usafiri bure kwa kila mteja ambaye anahitaji bidhaa kuletewa kutoka kwangu. Huduma hii ya kuletewa itakua kuanzia kilo tano na kuendelea kulingana na utafiti ambao nimefanya kupitia maeneo tofauti nimegundua kuwa kuna nafasi ya kufikia malengo yangu ikiwa nitaweza kupata Mtaji kuweza kwenda kununua bidhaa shambani na kuzileta sokoni.
Ninaomba kupitia Shooga.me kupata msaada wako ili niweze kufikia malengo yangu ya kukuza biashara yangu. Mungu akubariki.
ASANTE SANA!
Use the Moovn App to Scan this QR Code and Donate to this Campaign with
MoovnPay!